Mshambuliaji
asiye isha visa Mario Balotelli ambaye saivi amesajiliwa na klabu ya
Nice ya Ufaransa amesema kujiunga na Liverpool, ‘ulikuwa uamuzi mbaya
zaidi aliowahi kuufanya maishani mwake’.
“Isipokuwa mashabiki, ambao hunishabikia, na wachezaji kadhaa ambao tunasikilizana, sipendi klabu yenyewe,”
Balotelli ameiambia runinga ya Ufaransa ya Canal Plus.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 26, alisema hayo kabla ya kufunga mabao
mawili katika mechi yake ya kwanza na klabu ya Nice katika michuano ya
Ligue 1 walipofunga mabao 3-2 dhidi ya Marseille siku ya Jumapili.

No comments:
Post a Comment