Serikali
imesema kuwa bado inaendelea na tathimini ya kazi kwa watumishi wa umma
na punde itakapokamilika, itapanga mishahara na motisha upya kwa
watumishi wote wa umma wakiwemo wa sekta ya afya.
Waziri wa nchini Ofisi ya rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchini Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala
Bora Mhe. Angela Kairuki ambapo amesema lengo la kuongeza mishahara na
motisha ni pamoja na kuwajengea mazingira mazuri ya kuwahudumia wananchi
na kwa weledi na uadilifu.
Mhe.
Kairuki kwa mwaka 2016/2017, sekta ya afya ndiyo iliyoongezewa mshahara
kwa kiwango kikubwa kushindwa watumishi walioko serikali kuu na walimu
hali ambayo imelenga kuboresha zaidi sekta ya afya na kuondokana na vifo
visivyo vya lazima.
Aidha
ametumia fursa hiyo kuwataka wataalamu wa afya na watumishi wote
kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia viapo na maadili ya kazi zao na
kusema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kwa kadri ya
uwezo wake wa kulipa utakavyoimarika

No comments:
Post a Comment