HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, imelikataa ombi la kuiomba
Mahakama hiyo iwapatie Kibali cha Kufungua mahakamani hapo ombi la
kuomba Mahakama hiyo iifute amri /uamuzi wa Inspekta Jenerali wa Polisi
Ernest Mangu ya kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa nchini
kwasababu ya dosari za kisheria .
Uamuzi huo ulitolewa Juzi na Jaji Kiongozi Fredinand Wambali wakati
Katika ombi Na. 52/2016 lililowasilishwa Mbele yake na Baraza la
Udhamini la Chadema lilokuwa kikitetewa na wakili wa kujitegemea Peter
Kibatara dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Inspekta Jenerali wa
Polisi waliokuwa wakitetewa na Mawakili wa serikali Haruna Matagane na
Daniel Nyakeha.
Jaji Wambali alisema mlalamikaji alikuwa na Maombi mawili.Ombi la kwanza
Chadema ilikuwa ikiomba Mahakama hiyo iwapatie Kibali cha Kufungua Kesi
ya kupinga amri na uamuzi wa IGP wa Kuzuia mikutano na maandano ya
vyama Vya siasa nchini na ombi la pili waliomba Mahakama hiyo itoe tamko
la Kusema amri na uamuzi Huo wa IGP Si halali kisheria.
Uamuzi huo ulitolewa Juzi na Jaji Kiongozi Fredinand Wambali ambapo
alisema amekubaliana mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi
kwamba huwezi kuomba amri ya mapitio ya amri ya IGP Mahakamani hapo
wakati mlalamikaji alikuwa na Mlango mwingine wa kupinga amri ya IGP na
Mlango huo ni kwa mlalamikaji Kupenda kupinga amri ya IGP kwa Waziri wa
Mambo ya Ndani na alishindwa kufanya hivyo.
" Chadema walipaswa kukatia rufaa amri hiyo ya IGP ya Kuzuia maandamano
ya vyama Vya siasa Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na sio kwenda kushitaki
mahakamani' alisema Jaji Wambali na hiyo ikapatikana Katika Kifungu Cha
43(6) sura 322 ya Mwaka 2002 ya Judicial Review .
Aidha Jaji Wambali alisema anakubaliana na pingamizi la pili la Mawakili
wa serikali ambalo lilidai Kuwa ombi Hilo la Chadema litupwe kwasababu
ombi Hilo la Chadema halikuambatanishwa na maelezo ya mlalamikaji na
hayo maelezo yakidhi matakwa ya Kanuni ya 5(2) of The Judicial Reviews
Rules of 2014 ambayo inataka hiyo hati ya mlalamikaji ifafanue maelezo
na jina la mlalamikaji.
" Chadema Katika shauri Hili hayo yote walishindwa kuyafanya hivyo
Mahakama hii inatupilia Mbali ombi Lao la kutaka Mahakama hii itamke
amri ya IGP Kuzuia maandamano ni batiri kwa gharama kwasababu ombi la
Mlalamikaji halijakidhi matakwa ya kisheria.

No comments:
Post a Comment