WAKATI Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiapishwa jana Ikulu,
Dar es Salaam, baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wameshangazwa kuona
viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakidai kuwa
anaingilia kazi za jiji hilo.
Mkazi wa jiji hilo, Ismail Isaac alisema tatizo ni siasa za chuki kati
ya Chadema dhidi ya RC Gambo na kutaka wamuache afanye kazi kwani
wananchi wanamkubali, hivyo kama chama hicho cha upinzani hakimkubali,
kitajua chenyewe.
“Wananchi wanahitaji maendeleo sasa huu ushawishi wa Chadema kwenda kwa
wenyeviti wa mitaa unatoka wapi? Huyu Gambo anafanya kazi, sasa vikwazo
ni vya nini?” Alihoji Isaac na kusema kuwa Chadema inapaswa kutumikia
wananchi na si maneno.
Aidha, alimpongeza Rais John Magufuli kwa kumteua Gambo.
Aliwashangaa madiwani wa Chadema wanaotaka siasa za chuki ambazo
wananchi hawapo tayari kuzikubali. Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe, alisema Arusha
kuna siasa nyingi hivyo ni vyema viongozi wakatimiza majukumu yao ya
kikazi na kutokatishwa tamaa

No comments:
Post a Comment