Rais John Magufuli
ameshauriwa kukaa na vyama vya upinzani ili kutafuta mwafaka kabla ya
Septemba Mosi, siku ambayo Chadema imepanga kuanza operesheni inayoitwa
Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).
Ushari huo umetolewa na baadhi ya wasomi waliobobea katika taaluma mbalimbali nchini.
Chadema imesema
operesheni hiyo, itakayofanywa kwa maandamano na mikutano ya kisiasa
kote nchini, inalenga kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu,
ukandamizaji wa demokrasia na kutofuata Katiba na sheria.
“Ushauri wangu ni pande
mbili zinazovutana, zikae meza moja kutatua tatizo hilo. Mimi naamini
hakuna jambo zito hapo,” amesema Profesa Bakari Mohamed ambaye ni
mhadhiri wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa George Shumbusho amasema:
“Namwomba Mungu amtokee Rais Magufuli ili awaite wapinzani wazungumze yaishe.”

No comments:
Post a Comment