Wafanyabiashara waliokuwa wakitoka mnadani wamevamiwa na majambazi
yapatayo 10 ambayo na kumuua kwa risasi dereva aliyegoma kuwapa fedha na
simu.
Dereva huyo, Chrispin Inyangwe (40) alipigwa risasi ya mgongoni alipojaribu kupambana nao.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la katikati ya vijiji
vya Miula na Kalundi vilivyopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema wafanyabiashara
hao walikuwa wakitokea mnadani na walipofika eneo hilo walikuta mawe
yamepangwa barabarani kuzuia magari.
Amesema baada ya kuona mawe hayo, magari hayo yalilazimika kusimama na
ndipo majambazi hao waliokuwa na silaha za moto, mapanga na marungu
walipoibuka na kufyatua risasi hewani na baadaye kutaka wafanyabiashara
hao wasalimishe fedha na simu zao za mkononi.

No comments:
Post a Comment