Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amepongeza uteuzi
uliofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli ambapo alimteua Dk. Emmanuel
Nchimbi kwa Balozi.
Akizungumza na gazeti la Jamboleo, Edward Lowassa aliyekuwa miongoni mwa
watia nia wa Chama cha Mapunduzi alisema kuwa ni jambo jema
kushirikisha viongozi kuongoza nchi huku akibainisha kuwa mbali na
uteuzi wa Dk. Nchimbi pia kuteuliwa kwa mabalozi wengine nako
kumemfurahisha.
Wakati Lowassa akisifia uteuzi wa Dk. Nchimbi, wachambuzi wengine wa
masuala ya kisiasa walisema kuwa uteuzi huo unalenga kumaliza mvutano wa
muda mrefu na mgogoro ulioibuka ndani ya CCM wakati chama hicho
kikitafuta mgombea atakaye peperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu
mwaka jana.
Dk. Nchimbi ni mwanachama wa CCM ambaye alikuwa ni mwanamkakati katika
kambi ya Lowassa wakati wa mbio zake za kuwania kuteuliwa na chama hicho
kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Lowassa aliliambia gazeti la Jamboleo kuwa Dk. Nchimbi alikuwa
akionekana kama msaliti ndani ya chama hicho, lakini anaamini kufuatia
uteuzi huu shutuma hizo zitapungua. Aidha, alimsifia Dk. Nchimbi na
kusema ni kiongozi mwenye uzoefu

No comments:
Post a Comment