Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi
wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo
silaha za vita na sare za polisi.
Vitu hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya ujambazi.Inadaiwa
kwamba watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha katika jengo la Sophia
House lililopo Keko Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na
kutumia gari ya Noah.
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba watu hao ni pamoja
na mwanamke mmoja aliyekamatiwa Bunju katika Manispaa ya Kinondoni
ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na wanaume wawili waliokamatiwa
Mbagala Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.
Chanzo hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa ni pamoja na bunduki
tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake 526, panga
moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..
Vitu vingine ni pingu za chuma 45 na tatu za plastiki, ‘radio call’
12 , kamera ya CCTV moja, gari moja ya Noah, sare ya polisi jozi
moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.

No comments:
Post a Comment