Najua headlines za vilabu vya Simba na Yanga kuombwa kukodishwa na Simba
kununuliwa na bilionea wa 21 Afrika Mohammed Dewji ziligusa watu wengi
na kila mmoja kutoa mawazo yake akiwemo mwanasiasa na mbunge wa Kigoma
mjini Zitto Kabwe, Ayo TV ilimpata kwenye exclusive interview na kueleza
kwa kina kwa nini alipendekeza Mohammed Dewji apewe asilimia 40 na sio
51 kama ambavyo anataka:
“Timu zetu hizi ni timu za watu kwa hiyo ni lazima mipango yoyote ya uboreshwaji wa timu isinyang’anye watu timu, hawa watu wamewekeza kwa muda mrefu katika timu zetu hizi zenye miaka zaidi ya 70, kwa mfano MO anatakiwa kupewa sio zaidi ya asilimia 40 ili akitaka kufanya maamuzi ashirikishe wanahisa wengine na sio kumpa 51 awe anafanya maamuzi peke yake”

No comments:
Post a Comment