Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa
Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa
kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana
msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo
wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima
nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio
tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio
mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.
Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of
law) ambapo inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na
kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!.
The Separation of Powers & Check and Balance .
Nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge
(The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii mitatu,
ilipaswa kufanya kazi kwa kujitegemea bila mhimili mmoja kuingilia
mhimili mwingine (independence), huki kila mhimili uki act as a watchdog
wa muhimili mwingine usivuke mipaka ya madaraka au mamlaka yake yaani
(The sepaation of powers check and balance).
Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu
mihimili yao. President ndio mkuu wa the executive, Spika ndio mkuu wa
The Legistlatue, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja
na nia njema kuwa mihimili yote inamamlaka na hakuna mhimili wowote
uliokuwa unapaswa kuwa na mamlaka kuliko mhimili mwingine, lakini
kiukweli, mhimili wa the executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo
vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa the
executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!.
Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja
au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba,
mhimili wa Bunge na Mahakama ilipaswa kuingilia kati kwa kumcheck mkuu
wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais
ajisikie kuwa he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always
right!".
Udikiteta wa Magufuli.
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni
dikiteta wa ukweli ambaye hana msalie mtume, na alipoingia tuu
madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia
bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la
watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake
kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali,
likiwemo bunge na mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge
wakapige magoti kwa rais kuomba kutimiza wajibu wao!.
Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa
Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the
independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa
kujisubmit chini ya the executuve, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za
nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na
Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama,
lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive,
hivyo kumfanya rais ndio kila kitu!.
Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama,
wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo
nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye
kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!.
Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu
udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli ni dikiteta mzalendo!, mwenye
uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo
wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye
lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia
uchumi wa gesi na viwanda.

No comments:
Post a Comment