Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa
Tanzania Job Ndugai, amesema anasikitishwa na Wabunge wa UKAWA na Tabia
yao ya kutoka Nje. Japo ni haki yao kutoka nje lakini hivi karibuni
imezidi. Japo itaendelea hivi tutakuwa hatujengi nchi amesema.
Ameahidi yeye mwenyekiti wa Bunge na naibu Spika watakaa na UKAWA
wamalize hili tatizo kwani haipendezi spika unakaa mtu anatoka nje.
Amesema Sasa Nchi hii Migogoro, utengano umezidi, ni jukumu letu kama Viongozi kumaliza hii hali.
Kasema Wabunge waliofungiwa ilitokana na matomeo ya sintofahamu. Kwani
kabla ya kufungiwa tunaomba Mbunge afute kauli yake, arekebishe au alete
ushahidi. Pale anapokaidi huitwa kutoa ushahidi lakini saa nyingine
hukataa. Mfano kuna Mbunge alisema polisi wameleta Magari ya Washawasha
700. Tulipomwambia alete ushahidi akasema alisoma Kwenye JamiiForums.
Kama bunge hatuwezi fanya kazi kwa kutengemea Mitandao
Anasema hii hali inayoendelea bungeni inachochea chuki na Migogoro. Ni bora sasa tukaa nchini kama taifa ili tumalize hii hali.
Anasema kama Spika hatavumilia vijembe na kejeli kuendelea Bungeni
Ni haki ya mbunge kutoka nje. Lakini wale waliobaki nao wanawashambulia
waliotoka, hili nalo ni tatizo. Wabunge wakitoka nje mambo mengi
huharibika. Inachafua hali ya hewa. Uchaguzi unapoisha, siasa huhamia
Bungeni.
Tunachukulia Mbunge kama mtu mzima. Chama tawala na UKAWA na sisi tukae chini tuongelee hili swala.
Wabunge wamezoea kuona Spika na Naibu wake wakiwa wabunge wa
kuchaguliwa, hii ya naibu Spika kuwa wa kuteuliwa wanahofu kwamba
atakuwa anapokea maelekezo kutoka Sehemu Fulani. Naomba niwahakikishie
kwamba, sisi hatupokei maelekezo kutoka sehemu yoyote bali tunatoa
maamuzi yetu tunavyoona inafaa. Hivo watuamini

No comments:
Post a Comment