Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete leo ametoa tamko la Timu ya
Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola la Uchaguzi Mkuu wa Zambia
uliofanyika tarehe 11 Agosti, 2016 kuchagua Rais, Wabunge, Mameya,
Madiwani na Kura ya Maoni ya Katiba.
Rais Mstaafu Kikwete yuko nchini Zambia kufuatia Katibu Mkuu wa Jumuiya
ya Madola kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo yenye waangalizi wa
kimataifa 17 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.
Kwa mujibu wa tamko hilo, Jumuiya ya Madola imejiridhisha kuwa zoezi la
upigaji kura, usimamizi wa kura na uhesabuji kura vituoni kwa ajili ya
umeendeshwa kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa
chaguzi.
Tamko linasema, dosari na hitilafu zilizojitokeza hazikuwa kubwa kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu huo.
Amewapongeza wananchi wa Zambia kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa
amani na kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Amewasihi viongozi wa kisiasa wa Zambia, wagombea na vyama vya siasa
kuheshimu maamuzi wa wananchi na pale inapojitokeza upande wowote
kutoridhika na matokeo, zitumike njia za amani na kisheria za kutafuta
ufumbuzi.

No comments:
Post a Comment