RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake
umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini
Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment